Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Deco amekiri kuwa haitawezekana kuchukuliwa kwa nafasi ya Gavi aliyejeruhiwa kwenye soko la usajili na akapuuza uvumi kuwa klabu hiyo itatafuta kiungo mpya mwezi Januari.
Msimu wa Gavi wa 2023/24 huenda ukamalizika baada ya kurarua ACL yake na kuharibu meniscus wakati wa ushindi wa 3-1 wa Uhispania nyumbani dhidi ya Georgia katika mechi ya kufuzu kwa Euro 2024 Jumapili.
Ripoti zinadai kuwa Uhispania wanasitasita hata kumwita Gavi tena hadi 2025 baada ya kukasirisha Barcelona kwa kumchezesha kwenye mechi za raba.
Barca, hata hivyo, wana hatia ya kumfanyia kazi kupita kiasi kinda huyo mwenye umri wa miaka 19, huku kiungo huyo akicheza michezo 111 kati ya 121 ambayo wamecheza tangu alipocheza mechi yake ya kwanza mwaka 2021.
Huku Gavi sasa akitarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu, Barcelona wamepigiwa upatu kujaribu kutafuta mbadala wake wa muda katika dirisha la Januari, huku Thiago Alcantara wa Liverpool na Giovani Lo Celso wa Tottenham Hotspurs wakiwa miongoni mwa viungo wanaohusishwa na uhamisho wa kwenda Catalonia.