Kijana mmoja raia wa Urusi amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela baada ya kujaribu kuchoma moto vituo viwili vya kuwasajili wanajeshi wa Urusi.
Yegor Balazeikin, 17, alikiri kuhusika na mashambulio ya uchomaji moto katika ofisi za uandikishaji huko St Petersburg na Kirovsk, mji ulio umbali wa maili 21 kuelekea mashariki.
“Siwezi kukubaliana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine,” aliwaambia waendesha mashtaka.
“Kwa hiyo, nilianza kuzungumza na watu waliokuwa karibu nami ili kukusanya habari kuhusu usajili wa jeshi na ofisi ya uandikishaji.
“Niligundua kwamba mazungumzo hayakuwa na maana, na niliamua kwamba jambo fulani lilihitaji kufanywa ili kubadili hali hiyo.”
Balazeikin amewashutumu maafisa wa usalama wa Urusi kwa kutishia kumpiga na kumbaka akiwa kizuizini.