Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa nchini Marekani yanaonyesha kuwa Robert F. Kennedy Jr, mgombea binafsi wa uchaguzi wa rais utakaofanyika mwakani amewapita wagombea mashuhuri wa vyama vya Democratic na Republican.
Uchaguzi ujao wa rais wa Marekani utafanyika Novemba 2024.
Shirika la Habari la IRNA limeripoti leo kuwa, kulingana na takwimu zilizopatikana kutoka Kituo cha Taaluma za Siasa cha Marekani katika Chuo Kikuu cha Harvard na uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya Harris, asilimia 52 ya wapiga kura wa Marekani wanamkubali Robert F. Kennedy Jr., mgombeaji binafsi wa uchaguzi wa 2024, huku 27% tu kati yao wakisema hawavutiwi naye.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa maoni, kwa kujipatia alama 25, Kennedy ana kiwango cha juu zaidi cha uungaji mkono wa wapigakura.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa: Robert F. Kennedy Jr. ana kiwango cha juu zaidi cha umaarufu kulinganisha na Donald Trump na Joe Biden
Hii ni kwa kuzingatia kuwa 51% ya waliotoa maoni yao wameonyesha kuwa na mtazamo mzuri na 44% wamonyesha kuwa na mtazamo mbaya juu ya Trump.