Muigizaji wa Marekani Jamie Foxx ameshtakiwa na mwanamke anayedai kuwa alimnyanyasa kingono katika mgahawa mmoja huko New York City miaka minane iliyopita.
Kulingana na kesi hiyo, Bw Foxx, ambaye jina lake halisi ni Eric Marlon Bishop, alimpapasa mwanamke huyo ambaye jina lake halikutajwa baada ya kuomba apigwe picha naye.
Mshtakiwa anamtuhumu bwana Fox kwa unyanyasaji wa kingono.
Wawakilishi wa Bw Foxx hawakujibu ombi la BBC la kutoa maoni yao.
Kesi hiyo inadai kuwa shambulio hilo lilitokea mwendo wa saa 01:00 asubuhi mnamo tarehe 26 Agosti 2015 katika eneo la Catch NYC baada ya mwanamke huyo kuketi kwenye meza karibu na Bw Foxx.
Muigizaji huyo alionekana amelewa na kukubaliana na picha, akisema, “hakika kipenzi, nitafanya chochote kwa ajili yako”, kesi inasema.
Inaongeza kuwa alimwambia mwanamke huyo kuwa alikuwa na “mwili wa mwanamitindo” na ananukia “vizuri sana”.
Alimpeleka hadi sehemu iliyojificha ya mkahawa huo na kumshika matiti na kuweka mikono yake kwenye nguo yake ya ndani bila ridhaa yake, kesi hiyo inasema na kuongeza kuwa tukio hilo liliisha rafiki yake alipokuja kumtafuta.
Kesi hiyo pia inatafuta fidia kutoka kwa mmiliki wa mkahawa na baa Mark Birnbaum, ambaye mshitaki anasema alikuwa ameketi na Bw Foxx muda mfupi kabla ya shambulio hilo linalodaiwa kutokea.