Mkuu wa Mkoa Morogoro ameitaka jamii kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi pamoja na kua na mwamko wa kupima afya mara kwa mara ili kutambua afya zao.
Rc Malima ameyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisi kwake kwenye maandalizi ya maadhimisho ya siku ya ukimwi Dunia yanayotarajiwa kuanza novemba 24 na kilele kufikia disemba mosi mwaka huu ambapo kitaifa yatafanyika mkoani Morogoro.
Mhe.Malima amesema licha ya elimu kuendelea kutolewa lakini kumekua na baadhi ya watu wakihofia kupima afya pamoja na wenza wao huku wakiishi bilaa kutambua afya jambo ambalo linachangia kuongezeka kwa mamabukizi ya HIV
Amesema kupata maambukizi ya VVU sio mwisho wa maisha na sio hukumu ya kifo kwani utaendelea kufanya kazi kama kawaida kwa kuzingatia utaalamu unaotolewa na madaktari.
Kwa upande wake Emanuel Msinga makamu mwenyekiti baraza la watu wanaishi na virus Vya Ukimwi amesema bado kuna kundi wa watu hasa vijana hawajitokezi kutumia dawa ARV pindi wanapokutwa na VVU na kuendela kuambukiza watu wengine
Anasema uwepo wa dawa za ARV umesaidia kundi hilo kuimarika kiafya kwa WAVIU imekua ikipunguza kasi ya magonjwa nyemelezi huku wakiendelea na shughuli za uzalishaji kama kawaida.
“tunaishukuru serikali kwa kuendelea kujali afya. zetu kwa kutupatia bure dawa za ARV tutaendelea kutoa elimu kwa WAVIU ili kuona umuhimu wa matumizi ya dawa”
Naye mkazi wa. Morogoro aliyejitambulisha kwa jina la Abeid Kunani amesema kwa sasa elimu kwa jamii imeongezeka tofauti na zamani kuhusu ufahamu wa masuala ya HIV na umuhimu wa kupima afya .
Anasema siku za nyuma jamii ilikua ikimtenga kwa kutomsogelea hata kula pamoja mwenye HIV wakiogopa kuambukizwa jambo ambalo halina ukweli wowote .
Siku ya UKIMWI duniani inatarajiwa kuanza kufanyika novemba 24 na kilele kufikia Desemba mosi mwaka huu huku shughuli mbalimbali zikifanyika ikiwemo upimaji wa afya wa hiyari,michezo huku katika kilele mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa Majaliwa.