Meli nne za mafuta na nyingine nne zilizobeba gesi ya kupikia zimewasili kusini mwa Gaza, Jeshi la Ulinzi la Israel limesema.
Uwasilishaji huo ni sehemu ya mapatano ya muda yaliyokubaliwa kati ya Israel na Hamas.
Ingawa hakujawa na tamko rasmi la kuanza kwa siku nne za kusitisha mapigano, kuwasili kwa malori ya misaada huko Gaza ni ishara kwamba inaendelea.
IDF ilisema mafuta na gesi zilihamishwa kutoka Misri hadi kwa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa kupitia kivuko cha mpaka cha Rafah.
“Hili liliidhinishwa na serikali ya Israel kama sehemu ya kusitisha na mfumo wa kuachiliwa kwa mateka, kama ilivyokubaliwa na Marekani na upatanishi wa Qatar na Misri,” iliongeza.
Hapo jana, Hamas ilisema lori nne zitapeleka mafuta na gesi ya kupikia katika eneo hilo kila siku ya kusitisha mapigano.
Malori 200 ya ziada ya misaada yataingia Gaza kila siku kupeleka “msaada na vifaa vya matibabu”, iliongeza.