Imeelezwa kuwa Katika Mkoa wa Geita Vifo kwa Mwaka 2015_ 2016 Vimepungua kutoka Vifo 556 mpaka kufikia 104 hii imetokana na Jitihada zilizofanywa na Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo amesema Mipango ya Serikali ni kuhakikisha vifo vinapungua hasa kwa Wamama wajawazito wakati wa Kujifungua ndani ya Mkoa .
Hayo yameelezwa na Mganga Mkuu Mkoa wa Geita Dkt.Omari Sukari wakati wa Makabidhiano ya Gari la Kubebea wagonjwa katika kituo cha Afya cha Masumbwe ambapo amesema mpaka kufikia Mwaka 2030 vifo kwa vizazi hai 100000 vitakuwa vimefikia 70 ndani ya Mkoa wa Geita huku akisema uletwaji wa Magari ya Kubebea wagonjwa utapelekea kupunguza Vifo.
“Walikuwa angalau akina Mama 556 kati ya Vizazi hai 100000 lakini Baada ya Jihada mbalimbali za Serikali na uwekezaji angalau Vifo vimepungua kutoka 556 mpaka Vifo 104 lakini lengo la Serikali Mh Mkuu wa Mkoa ni kupunguza Vifo hivi itakapofika Mwaka 2030 angalau vifikie Vifo 70 kwa Vizazi hai 100000, ” Dkt.Sukari.
Akikabidhi Gari hilo Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela akiambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati katika ziara ya kukagua na kutembelea Miradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Shigela amewataka watumishi wa Afya kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa wananchi pamoja na Matumizi mazuri kwa Gari liloletwa kituoni hapo.
Mohamed Gombati ni Katibu Tawala Mkoa wa Geita amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Magari ya kubebea wagonjwa kwa wananchi nakwamba yataenda kusaidia sehemu zilizo na Changamoto katika Vijiji sambamba na kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe kuhakikisha analifanyia huduma mara kwa mara