Jumuiya ya wanafunzi vyuo vikuu Tanzania ( TAHLISO ) imewaasa wanafunzi wanao kwenda likizo ndefu ya Mwezi Desember, kuwa waangalifu wanapo kuwa mazingira ya nyumbani na kujiepusha na vishawishi Mbalimbali vinavyoweza kuleta athari katika masomo yao.
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana Nganza Jijini Mwanza Rais wa jumuiya hiyo Maria Thomas amesema wameamua kutoa Somo kwa wanafunzi shule kwa shule lengo ni kuunga juhudi za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan za kumlinda na kumsaidia mtoto wa kike anapo kuwa katika mazingira ya Shule na ya nyumbani.
Kamishina wa jinsia, ustawi wa jamii na maendeleo ya wanawake (TAHLISO) Hawa Laurence amewaasa wanafunzi kuacha tamaa na kuepuka mitindo ya maisha ambayo haikubaliki ndani ya jamii zetu.
Nae makamu wa Rais Chuo kikuu CUHAS – Bugando Glory Kiroche amewaasa wanafunzi kusoma kwa bidii na kuwa na nidhamu kwani nidhamu ndio kichocheo cha mafanikio kwao.