Mkuu wa kitengo cha habar jumuiya ya wanafunzi africa mashariki (EASU) Eng Aman mdekha ameshiriki na kutoa salamu za jumuiya ya wanafunzi Africa mashariki (EASU) katika mkutano mkuu wa kwanza wa Jumuiya ya wanafunzi taasisi za elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) uliofanyika katika chuo kikuu cha iringa.
ambapo yalijadiliwa mambo kadha wa kadha yanayohusu mstakabali mpana wa vijana wa vyuo na vyuo vikuu nchini Tanzania,kiongozi huyo amemushukuru sana Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania kwa kazi nzuri anayoifanya katika kuwatengenezea wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu mazingira rafiki ya kujifunzia .
“ namupongeza sana Rais wa Jamuhuri Ya muunganowa Tanzania dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofainya katika kuwatengenezea wanafunzi mazingira rafiki ya kusoma na kujifunzia ikiwemo kuendelea kutoa mikopo kwa wakati kwa wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu na kutoa ufadhili kupitia samia scholarship hakika kiukweli anafanya kazi nzuri sana na kama wasomi tuna kila sababu ya kumuunga mkono “
kiongozi huyo amesema jumuiya iyo ya wanafunzi ipo katika mchakato wa kuandaa hafla maalumu ya kuwaribisha rasmi wanafunzi wa Somalia kupitia shirikisho la vyuo na vyuo vikuu nchini humo katika jumuiya ya wanafunzi Africa mashariki.