Shirika la afya duniani, WHO limeeleza wasiwasi wake kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Monkeypox nchini DRC, zaidi watu 581 wakiwa tayari wamefariki kutokana na ugonjwa huo.
Wagonjwa zaidi ya 13, 000 wameripotiwa kuugua ugonjwa huo wa monkeypox, mamlaka za afya nchini humo zikihusisha ukosefu wa pesa kuwa chanzo kikuu cha kusambaa kwa ugonjwa huo kwa kasi.
Ugonjwa huo umeathiri mikoa 21 kati ya 26 nchini DRC, mikoa ya Équateur, Sankuru, Maï-Ndombe na jiji la Kinshasa ikiathirika ziadi.
Afisa wa serikali ya Kinshasa anayehusika na hali ya dharura, Cris Kasita, amesema serikali inahitaji Dolla millioni 4, kukabili hali ya ugonjwa huo katika mikoa mine iliyoathirika zaidi.
WHO sasa inahofia kuwa iwapo hali hiyo hatathibitiwa basi huenda mataifa jirani pia yakaathirika.
Ugonjwa huo unadaiwa kusambazwa na mtali kutoka Ubelgiji aliyezuru DRC mwezi machi mwaka huu.