Shirika la Afya Duniani, WHO limeripoti siku ya Jumamosi visa 12,569 vinavyoshukiwa kuwa vya ugonjwa wa Ndui (smallpox), ikiwa ni pamoja na vifo 581, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia mwezi wa Januari hadi Novemba 12, idadi kubwa zaidi ya kila mwaka ya maambukizi kuwahi kurekodiwa.
“Hii ni idadi kubwa zaidi ya kesi zilizowahi kuripotiwa kwa mwaka mmoja, baadhi katika maeneo ya kijiografia ambayo hayajawahi kuripoti kesi za ugonjwa wa Ndui hapo awali, ikiwa ni pamoja na Kinshasa, Lualaba na Kivu Kusini,” kulingana na ripoti ya hali ya Shirika la Afya Duniani huko Geneva.
WHO ambayo inatiwa wasiwasi na aina mpya za maambukizi ya kingono ya clade (lahaja) I ya virusi, kwa sasa inaongoza misheni ya pamoja na Wizara ya Afya ya DRC “kutathmini hali” hiyo.
Ugonjwa huo – ulioripotiwa kwa mara ya kwanza kwa binadamu mwaka 1970 nchini DRC – una dalili ya upele wa ngozi, ambao unaweza kutokea kwenye sehemu za siri au mdomoni, na unaweza kuambatana na milipuko ya homa, koo au maumivu kwenye nodi za limfu.
Mlipuko wa ugonjwa wa Ndui (smallpox) uligunduliwa, kuanzia Mei 2022, huko Ulaya na Marekani, mbali na nchi kumi za Afrika ya Kati na Magharibi ambapo ugonjwa huo umeenea kwa muda mrefu, na hivyo kusukuma WHO kutangaza kiwango cha juu cha tahadhari mnamo Julai 23, 2022.
Mnamo Mei 11, WHO iliondoa tahadhari hiyo, huku ikitoa wito kwa watu kuwa macho.