Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mh. Mohamed Mchengerwa amewataka viongozi wa serikali kuwa na utaratibu wa kurudisha kwa jamii na kujitolea kwa wananchi bila kusubiri bajeti za serikali, Mh. Mchengerwa amesisitiza viongozi kujitoa kwa wananchi na kuwasaidia shida zao kwa kusema kuwa kiongozi hasiyejua shida za wananchi na kuzitatua kiongozi huyo hafai
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa ofisi ya serikali ya mtaa wa Mkunguni wilaya ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam Ofisi hiyo ya kisasa ambayo imetengenezwa kwa kujitolea na Diwani wa kata ya hananasif Kinondoni Dar Es Salaam Mhe Wilfred Nyamwinja.