Chama Cha Mapinduzi (CCM ) kimetoa taarifa ya kufanyika kwa vikao vya kawaida vya uongozi ngazi ya Taifa kuanzia November 27, 2023 hadi November 29, 2023 Jijini Dares salaam.
Akiongea leo Jijini Dar es salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda @baba_keagan amesema “Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ataongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa (NEC) vitakavyoketi tarehe 29 Novemba 2023, jijini Dares salaam”
“Vikao hivyo vitatanguliwa a Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa iliyoketi November 27, 2023, ikifuatiwa na mafunzo (Semina) ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa tarehe 28 Novemba 2023”