Vijana watakiwa kujihusisha na Michezo mbalimbali kwa lengo la kuupa mwili nguvu mazoezi na kutojihusisha na makundi ya hualifu pamoja na athari za madawa ya kulevya.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti la Tanzania Leo, Frank Malaki wakati wa kufunga mashindano ya mpira wa miguu ya Upendo Super Cup yalioandaliwa na Umoja wa vijana Usharika wa Kanisa la Kiinjili la Kiruthel Tanzania Mabibo External.
Malaki amewataka vijana kuzidi kujikita zaidi kwenye mazoezi kuimarisha mwili, Umoja na mshikamano katika kristo kwa kudumisha upendo na amani.
Katika mchezo huo timu ya KKKT mtaa kisiwani imetwaa kombe la ushindandi la Upendo Super Cup baada ya kuwachapa Tabata Shule kwa mikwaju ya penati 8-7.
KKKT mtaa wa kisiwani wametwaa taji hilo baada ya mchezo kumalizika kwa sare ya bao moja kwa moja na ubingwa kuamuliwa kwa mikwaju ya penati na kutwaa Kombe, jezi na mpira huku washindi wa pili wametwaa zawadi ya jezi pamoja na mpira.
Kwenye mashindano hayo Boko Ushirika waliibuka washindi wa tatu baada ya kuwafunga waandaaji wa mashindano hayo Mabibo External kwa mikwaju ya penati 6-5.
Edwin Mbiza mshambuliaji wa Mabibo External aliibuka kuwa kirara mfungaji bora wa mashindano hayo baada ya kupachika mabao matano nyavuni huku kipa wa mabingwa wa michuano hiyo Robart Masala akiibuka kipa bora wa mwaka.
Bingwa wa mashindano hayo alitwaa taji, mbuzi, mpira na seti moja ya jezi, huku mshindi wa pili ambaye akiwa ametwaa jezi pamoja na mpira baada ya kuchapo alipata seti ya jezi na mpira mmoja na mshindi wa tatu alipata jezi na mpira.
Kwa upande wake Mchungaji wa kanisa hilo, Imani Hatibu amesema kuwa lengo la kuandaa michuano hiyo ni kuwaunganisha Vijana ni nguvu ya kazi ya kanisa na taifa inasaidia kushirikiana na kuonyeshana vipaji vyao hasa katika kuunga jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuinua michezo na kuchana na uhalifu katika jamii.
“Michuano hii imeandaliwa na umoja wa vijana katika makanisa yetu na lengo ilikuwa ni kuwaleta pamoja vijana wote sambamba na kuunga mkono juhudi za mama katika kuinua michezo,” amesema.
“Michuano hiyo ufanyika kila mwaka ilikusaidia zaidi vijana kutoshawishika kiingia kwenye makundi mabaya ambayo hayatakuwa na msaada kwao na kwenye jamii ila kubadilishana mawazo kuongeza mtandao wa vijana wanaomjua neno la Mungu.”
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Usharika wa KKKT Mabibo External Erick Kisaule amesema kuwa mashindano hayo wameandaa kwa lengo la kuwaunganisha vijana na kuubiri amani upendo naeushirikiano na uzalendo ni faraja kwetu kuwakutanisha vijana tangu mwezi wa 5 hadi leo kuhitimisha.