Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Tanga imekabidhi Vifaa mbalimbali vya Kielektroniki kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga ukiwa ni mchango kutoka ofisi ya Mamlaka ya mapato kama sehemu ya Mashirikiano mazuri na Taasisi za Serikali ikiwa pia ni Maandalizi kuelekea Wiki ya Mlipa Kodi inayotarajiwa kuanza November 30, 2023 hadi Tarehe 4, December 2023
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji amesema wamepokea Vifaa hivyo kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Tanga vitakavyosaidia kwa ajili ya Utunzaji wa kumbukumbu za Kiofisi na shughuli za Serikali.
“Vifaaa hivi kwa kweli vimefika muda muafaka ambavyo vitatusaidia sana katika maeneo yetu ya kazi, na hii itatusaidia katika kupambana na kuhamasisha wananchi na kutunza kumbukumbu wa ulipaji wa kodi” amesema James Kaji
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Tanga Thomas Masese vifaa hivyo ni sehemu ya mchango kutoka Mamlaka ya mapato mkoa wa Tanga ikiwa ni sehemu ya ushirikiano mzuri baina ya ofisi za Serikali pia ikiwa ni Maandalizi ya wiki ya Mlipa kodi.