Polisi nchini Sierra Leone wanasema wanaendelea na msako wa kuwatafuta watu wanaohusika na kile ambacho serikali imekitaja kuwa ni shambulizi lililopangwa na kuratibiwa katika mji mkuu huo.
Watu wenye silaha walivamia ghala la kuhifadhia silaha na magereza kadhaa mjini Freetown siku ya Jumapili, na kuwezesha karibu wafungwa 2,000 kutoroka.
Maeneo na vifaa muhimu nje ya mji mkuu pia vililishambuliwa.
Mamlaka inatoa zawadi ya $2,000 (£1,580) kwa yeyote aliye na taarifa kuhusu mhalifu ambaye bado yuko huru, pamoja na $1,000 kwa wafungwa waliotoroka.
Amri ya kutotoka nje usiku ingalipo kote nchini Sierra Leone.
Watu 20 walikufa katika mashambulizi hayo, 13 kati yao wakiwa wanajeshi watiifu kwa serikali.