Wakenya wataendelea kutozwa ushuru wa Nyumba baada ya Mahakama kutoa amri ya kwa serikali kuendelea kutekeleza sheria hiyo hadi Januari 10, 2024.
Haya yanajiri baada ya mahakama kutangaza tozo hiyo kuwa kinyume cha sheria, ikisema inakiuka Ibara ya 10, 2 (a) ya Katiba.
Amri za kusitisha kesi hiyo zinafuatia ombi la Walalamikiwa katika kesi hiyo wakiongozwa na wakili George Murugara kwa muda wa siku 45 ili kutekeleza uamuzi wa mahakama.
“Katika siku hizo 45, ninakuomba usitishe ukandamizaji wa matokeo hayo mahususi katika hukumu na amri yoyote ili kusubiri kuwasilishwa kwa maombi rasmi chini ya Kanuni za Mutunga na Kanuni za Mahakama ya Rufaa,”alisema Murugara.
“Sababu ni kwamba, kwanza, tunapaswa kufanya marekebisho yanayohitajika kwa utaratibu wa serikali wa kutoza ushuru ndiposa kusiwe na chama au shirika la serikali litakaloshotakiwa kwa dharau ,”aliongeza