Israel na Hamas wamefikia makubalino ya dakika za mwisho leo Alhamisi kuongeza sitisho la mapigano kwa siku ya saba , na Washington imesema inatarajia makubaliano hayo yanaweza kuongeza kuachiliwa kwa mateka zaidi na kupelekea misaada zaidi kufika Gaza.
Makubaliano yamepelekea baadhi ya misaada kibinadamu kuingia Gaza baada ya sehemu kubwa ya eneo la pwani lenye watu milioni 2.3 limekuwa kama nyika kutokana na wiki saba za mashambulizi ya Israel kulipiza kisasi shambulizi la mauaji la wanamgambo wa Hamas Octoba 7.
Wakati huo huo shambulizi la mauaji mjini Jerusalem lilikuwa ni ukumbusho muhimu kwa ghasia kusambaa.
Israel ambayo imedai Hamas iwaachilie walau mateka 10 kwa siku ili kuwezesha sitisho la mapigano kuendelea , imesema ilipokea orodha ya dakika za mwisho ya wale watakaoachiliwa leo na kuruhusu kusitishwa mpango huo wa kuanza tena mapigano alfajiri.
Hamas ambao iliwaachilia mateka 16 Jumatano wakati Israel imewaachilia wafungwa 30 wa paletsian pia imesema makubaliano yataendelea kwa siku ya saba.