Msanii wa nyimbo za Hip-hop Cardi B ameeleza kiasi cha pesa mashabiki wake wanazolipa wanapohudhuria shoo zake.
Nyota huyo wa Hiphop alidhibitisha kwamba bei ya shoo zake ni ghali mnokwa mashabiki wa kawaida.
Mama huyo wa watoto wawili alifichua kwamba asingeweza kuondoka nyumbani kwake kwenda kwenye tamasha ikiwa mwandalizi au promota hakuwa tayari kufikia tiketi ya sh153 Milioni na zaidi.
“Siwezi kutoka kwangu kuenda kutumbuiza ikiwa tikiti sio sh 153 milioni na zaidi Ikiwa mashabiki hawatalipa kiasi hicho basi sitoki,” alisema.
Hii si mara ya kwanza kwa nyota huyo kutangaza bei ghali ya show zake kwa mashabiki.
Mwaka jana, Cardi B alitumia akaunti yake ya X kwa kiasi kikubwa na kujivunia jinsi alivyotengeneza dola milioni 1 kwa onyesho la dakika 35 huko Miami.
Katika katika chapisho hilo la zamani, nyota huyo alieleza kuwa alitumbuiza takriban watu 400 katika hafla ya benki ya wasomi kabla ya kuwashauri watu wafikirie juu kuhusu gharama ya tikiti yake kabla hawajaanza kuzungumza naye kuhusu kufanya shoo.
“”Nililipwa dola milioni 1 ili kutumbuiza katika hafla ya mwanabenki mashuhuri.” Hafla hiyo ilifanyika kwa “watu 400 na kwa dakika 35 tu,” alichapisha.
Ingawa milioni 153 ni pesa nyingi sana, msanii huyo si mwanamuziki anayelipwa zaidi kwa hafla za maonyesho.