Mawakala nchini Uingereza hawatalazimika kuzingatia kanuni mpya za FIFA zinazozuia kiasi cha kamisheni wanachoweza kupata baada ya kuibua pingamizi la kisheria.
Haya yanajiri baada ya maajenti wenye makao yake nchini Uingereza kuungana ili kuzuia kutekelezwa kwa sheria hizo mpya kufuatia uamuzi sawa na huo nchini Ujerumani.
Wakala mmoja aliiambia talkSPORT: “Huu ni ushindi wa akili timamu na uhuru wa biashara.
“FIFA inafuata watu wasiofaa. Wanapaswa kuwabana vilabu na sio mawakala.”
Vilabu vya Premier League vilitumia zaidi ya £2bilioni kwa ada ya mawakala katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.
Sheria hizo mpya zilipaswa kuanzishwa nchini Uingereza kuanzia Oktoba 1, lakini zilisitishwa kufuatia changamoto ya kisheria kuzinduliwa.