Kampuni ya Afrika Kusini itatengeneza kifaa maalum kinachoingizwa ukeni kwa wanawake ili kujikinga na maambukizi ya VVU, ambacho wataalam wa UKIMWI wanasema kitapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu.\
Baraza la Idadi ya Watu lilitangaza siku ya Alhamisi kuwa Kiara Health ya Johannesburg itaanza kutengeneza kifaa hicho kinachojulikana kama ‘silicone ring’ katika miaka michache ijayo, na kukadiria kuwa vifaa milioni moja vinaweza kutengenezwa kila mwaka.
Kulingana na VOA vifaa hivyo hutoa dawa ambayo husaidia kuzuia maambukiz ya VVU na vimeidhinishwa na karibu nchi kadhaa pamoja na Shirika la Afya Ulimwenguni.
Baraza ambalo lisilo la faida linamiliki haki za vifaa hivyo, ambavyo sasa zinatengenezwa na kampuni ya Uswidi. Mpaka sasa takriban pete 500,00 zinapatikana kwa wanawake barani Afrika bila gharama, zinazonunuliwa na wafadhili.
Ben Phillips, msemaji wa shirika la U.N. UKIMWI, alisema faida ya kifaa hicho ni kwamba inawapa wanawake uhuru wa kuitumia bila mtu mwingine kujua au kutoa ridhaa.