Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa serikali kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI imeandaa Mpango Mkakati mpya jumuishi wa kuratibu Wahudumu wa afya ngazi ya jamii ambao utaajiri watoa huduma 137,294 ndani ya miaka mitano.
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo leo kwenye maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika Mkoa wa Morogoro.
“Kupitia mpango huu, tutasomesha na kuajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii wawili katika kila kitongoji, katika vitongoji vyote 64,384 tutakuwa na vijana ambao tutawapa mafunzo ya miezi 6 na tutawaweka kama sehemu ya watumishi rasmi wa Sekya ya Afya” amesema Waziri Ummy Mwalimu na kuongeza kuwa Serikali pia itaajiri wahudumu ngazi ya jamii wawili kila mitaa katika mitaa yote 4263.
Waziri Ummy amesema Wizara itaajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii 137,000 na hawa ndio watakuwa jeshi la afya katika jamii, na watapita nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, kitongoji kwa kitongoji kuhamasisha masuala mbalimbali ya afya.
Amesema kuwa Serikali imebainisha maeneo 6 muhimu ya kipaumbele ya usimamizii watakaofanya watoa huduma za afya ngazi ya jamii ambayo ni udhibiti wa Magonjwa ya kuambukiza, Kifua Kikuu na Malaria, Magonjwa yasiyoambukiza na Magonjwa mlipuko. Mengine yakiwa ni masuala ya Afya ya Uzazi, Lishe, Mama na Mtoto, Usafi wa Mazingira