Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani amekemea vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaojihusisha na wizi wa mifugo pamoja na ulaghai wa mali za wananchi katika kata ya Ukune na kuwataka kuacha mara moja kwa hiari kabla ya hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.
Cherehani ameyasema hayo wakati wa akikabidhi gari la wagonjwa katika Kata ya Ukune Jimbo la Ushetu ambapo amewataka viongozi waliopewa dhamana kuhakikisha wanashirikiana na wananchi katika kusimamia maendeleo ya wakazi wa eneo hilo.
Akiongea katika Mkutano huo ulioshirikisha Viongozi wa Chama cha CCM na wananchi wa eneo hilo Mbunge Cherehani amesema kuwa kumekuwa na kesi zinazoripotiwa za watu kupoteza mifugo yao, kubambikiwa kesi na kudhurumiwa mali ambapo amesema tayari majina ya wale wote wanaofanya matendo hayo ameshapelekewa na Serikali haitowavumilia na wasipokubali kuacha kwa hiari hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.