BAADA ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuzindua Mpango wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Wanawake wa Bara la Afrika, Mbunge wa jimbo la Rufiji mkoani Pwani ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEM) Mohamed Mchengerwa kwa kushrikiana na Oryx Gas ameamua kuunga mkono hatua hiyo kwa kugawa bure mitungi ya gesi ya Oryx 900 na majiko yake kwa Mama Lishe wote wa wilaya ya Rufiji.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman amesema wamefurahi kupeleka nishati safi ya kupikia kwa wananchi wa wilaya ya Rufiji na kugusa kundi hilo muhimu katika jamii ambalo shughuli zao za kila siku zinahitahi kupata nishati ya kupikia.
“Kupika katika gesi ya oryx ni kulinda mazingira kwa kuacha kukata miti na zaidi ya yote ni kulinda afya ya wanawake na watoto ambao wamekuwa wakiathirika kwa kuvuta moshi mbaya unaotokana na kuni. Rais wetu Mama Samia amejipanga kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata nishati safi ya kupikia ifkapo 2032.
“Katika mkutano wa Dubai ,Rais Samia amezindua Mpango wa Nishati safi ya kupikia kwa wanawake wa Afrika.Oryx Gas tutaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhamasisha matumizi ya nishati safi ua kupikia kwa kugawa bure mitungi ya gesi na majiko yake.