Katika kuendeleza mapambano dhidi ya utapiamlo katika mkoa wa Iringa Mkurugenzi wa idara ya sera na uratibu wa shughuli za serikali katika ofisi ya Waziri Mkuu , Paul Sandawe akiambatana na viongozi wengine kutoka wizara ya afya Ofisi ya Rais Tamisemi pamoja na Uongozi wa Shirika la Gain wamefanya ziara mkoani Iringa kuanzia Disemba 1 hadi 3 ikiwa na lengo la kuimarisha mapambano dhidi ya utapiamlo mkoani Iringa
Shirika la GAIN (Global Alliance for improved Nutrition) linakosaidia kutoa ushirikiank wa kimataifa wa kuboresha lishe , linaunga mkono juhudi za vyama hivi katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula chenye virutubishi muhimu na usalama , na linachukua nafasi muhimu katika kuboresha matokeo ya afya lishe nchini Tanzania .
Ziara hii ni sehemu ya mpango wa kutathmini maendeleo ya urutubishaji wa unga wa mahindi kwa wanufaika wa msaada wa kiufundi na vinyunyizi 50 zenye thamani ya millioni 70, vilizotengenezwa hapa nchini na kampuni ya PEC chini ya usimamizi wa SIDO na kugaiwa kwa vyama vya ushirika vya wasindikaji wadogo na wakati (SMEs) wa unga wa mahindi katika mikoa ya Iringa , Kilimanjaro , Manyara Mara na kagera .
Mpango huu unaendana na dhamira ya Gain ya kusaidia mifumo endelevu ya chakula na kuboresha upatikanaji wa mlo wenye lishe hususan kwa jamii zilizo hatarini , hivyo ziara hii ni ushuhuda wa juhudi za ushirikiano kati ya serikali na shirika la GAIN katika kushughulikia changamoto za lishe nchini Tanzania