Mbunge wa jimbo la Kilolo Mhe. Justine Nyamoga amesema kabla ya mwaka huu kuisha vijiji vyote katika wilaya ya kilolo Vitakuwa na umeme .
Nyamoga ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Nyanzwa , Mgowelo pamoja na Igunda na hii ikiwa ni sehemu ya miendelezo ya ziara zake katika wilaya ya kilolo na amesema kukiwa na umeme hii itachangia sana kukuza shughuli za kimaendeleo.
“ Wilaya ya kilolo ni miongoni mwa wilaya chache sana hapa Tanzania zenye umeme vijiji vyote na nimpongeze Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye ametoa fedha hizi ili nyinyi wananchi muwe na umeme na wakati naingia kulikuwa na vijiji 21 havina umeme ila hadi sasa tumebakiza vijiji viwili ambavyo hadi mwshoni mwa mwezi disemba vitakuwa na umeme “ Amesema Nyamoga
Vile vile Nyamoga amewataka viongozi wote wa serikali katika vijiji wawe waadilifu katika utumiaji wa pesa za wanannchi
“ Alafu pia niwaombe viongozi kuweni waadilifu katika matumizi ya fedha za wanannchi wanazo changa kwasababu msipokuwa waadilifu kwao kesho na kesho kutwa na wao watakosa moyo wa kuendelea kuchanga kwenye maendeleo mengine “ amesema Nyamoga