Rais wa Bayern Munich Herbert Hainer alisalia na imani kuwa Thomas Muller ataongeza mkataba wake huku kukiwa na tetesi za kujiunga na Manchester United.
Mkataba wa sasa wa mshambuliaji huyo mkongwe unamalizika Juni 2024 lakini mkuu wa Bayern Munich Herbert Hainer alidai kuwa klabu hiyo inawasiliana na mchezaji huyo na wana imani kwamba ataongeza muda wake wa kukaa kwa mwaka mmoja zaidi licha ya mchezaji huyo kuhusishwa na kuhamia Manchester United.
Mbali na kuhusishwa na Mashetani Wekundu, nahodha wa zamani wa Ujerumani aliyeshinda Kombe la Dunia Lothar Matthaus hivi majuzi alimshauri mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 kwamba afikirie kuondoka katika klabu hiyo ikiwa anataka kucheza mara kwa mara zaidi.
Alipendekeza zaidi kwamba Muller anaweza kufikiria kuhamia MLS ambapo anaweza kuungana na mpinzani wa zamani wa Ligi ya Mabingwa Lionel Messi.