Saudi Arabia imesajili baadhi ya majina makubwa katika soka msimu wa joto na ingawa wachezaji wengi walikubali kujiunga na vilabu vya ligi, baadhi walikataa.
Neymar Junior, Sadio Mane, na Karim Benzema walikuwa baadhi ya wachezaji waliomfuata Cristiano Ronaldo hadi SPL.
Kinyume chake, wachezaji kadhaa mahiri – akiwemo kiungo wa Real Madrid – walichagua kusalia Uhispania.
Kulingana na jarida la Uhispania la Marca, Federico Valverde alikuwa na ofa kutoka Saudi Arabia lakini alitaka kusalia Real Madrid.
Bayern Munich pia walitaka kumsajili Valverde, lakini raia huyo wa Uruguay alikataa uhamisho huo.
Uaminifu wa Valverde ulizawadiwa kwa mkataba mpya na wababe hao wa Uhispania hadi 2029.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amekuwa mchezaji muhimu wa Los Blancos na klabu inaonekana kumwona kama msingi wa enzi mpya.
Huku Luka Modric na Toni Kroos wakielekea kustaafu, Valverde anaonekana kama mbadala wake pamoja na Eduardo Camavinga na Aurelien Tchouameni.
Ameanza mechi 18 kati ya 20 alizocheza msimu huu, kulingana na Transfermarkt. Kufikia sasa, ameichezea Real Madrid zaidi ya michezo 200 na ameeleza nia yake ya kuwa nahodha.