Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya amewataka Watanzania kuwatumia Wataalamu pindi wanapofanya shughuli zozote hususani za ujenzi ambapo amesema wasipowatumia Wataalamu gharama yake itakuwa kubwa sana “Kama unajenga nyumba hakikisha imesanifiwa na Mtaalamu”
Akiongelea kuhusu athari za mafuriko kwenye maeneo mbalimbali nchini Kasekenya amesema hata pale Watu wanapojenga kabla ya ujenzi wa jengo lolote ni vizuri wakaenda kwa Watu wanaotoa vibali vya kujenga ambao watawaambia kama wanapotaka kujenga ni eneo sahihi au sio sahihi na sio salama kujenga “Ukiambiwa sio sehemu sahihi ukijenga maeneo hayo kimsingi umefuata tatizo sio tatizo linekufuata , wanaofuata majanga wapeuke hilo”
Amesema hayo wakati wa Ugawaji wa Tuzo za Ujenzi na Majengo Afrika Mashariki kwa Mwaka 2023 (EABC), zilizofanyika Katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam ambapo katika hatu nyingine amesema Serikali itaendelea kuwaamini Wakandarasi wa Ndani kwa miradi mbalimbali ikiwemo ile mikubwa ambayo wanaweza wakafanya vizuri kwani Serikali tayari imeongeza wigo mpana katika sheria ya manunuzi kwa lengo la kuwanufaisha Wazawa,
Kasekenya amesema wahandisi wanapaswa wapate vifaa bora ikiwemo Saruji, nondo, misumari, vigae, marumaru na bidhaa zote zinazotumika kwenye ujenzi ambazo zinazalishwa na kampuni hizo “Ukiwa Mhandisi mzuri halafu ukapata bidhaa zisizobora basi hautafanya chochote kizuri, moja ya kitu ambacho Serikali tunakitaka ni kuwa na vifaa na uhandisi bora hivyo tunatoa wito kwa wadau wanaojihusisha eneo hili kutoa huduma zilizobora ambazo zinaingia kwenye mnyororo mzima wa ujenzi”
Kwa upande wake Angela Leila Maingu Sales and Marketing Manager kutoka Modern Industrial Park ambao ni miongoni mwa Kampuni zilizopata tuzo, Anjella Leyla ameishukuru Serikali kwa ushirikiano unaozipa Taasisi na Mashirika mbalimbali ikiwemo mradi wao wa kongani ya viwanda vya kisasa Mkoani Pwani, Tuzo za Ujenzi na Majengo za Afrika Mashariki kwa Mwaka 2023 umeshindanisha makampuni zaidi ya 500 kwa lengo la kuongeza ushindani miongoni mwa wadau wa Sekta ya Ujenzi lakini pia kufanya chachu ya utoaji wa huduma bora katika mnyororo mzima wa Sekta ya Ujenzi.