Serikali ya Uganda siku ya Jumatano ilishutumu upanuzi wa Marekani wa vikwazo vya viza dhidi ya maafisa wake, ikiishutumu Washington kwa kusukuma “ajenda ya LGBT” barani Afrika.
Vizuizi vipya vya viza vilivyotangazwa Jumatatu vinalenga maafisa wasiojulikana ambao Marekani inawaona wana jukumu la kudhoofisha demokrasia na kukandamiza makundi yaliyotengwa nchini Uganda, ikiwa ni pamoja na jumuiya ya LGBTQ.
Uganda ilipitisha mojawapo ya sheria kali zaidi duniani dhidi ya mashoga mwezi Mei, ambayo inataka hukumu ya kifo kwa baadhi ya vitendo vya jinsia moja.
Marufuku ya kusafiri ilitangazwa Jumatatu na kuwalenga maafisa ambao hawakutajwa ambao Marekani inahisi wanawajibika katika kuhujumu demokrasia na kukandamiza watu wa tabaka la wachache nchini Uganda, ikiwa ni pamoja na jamii ya LGBT. Uganda ilipitisha moja wapo ya sheria kali kabisa duniani dhidi ya wapenzi wa jinsia moja mwezi Mei ambayo inahitaji adhabu ya kifo miongoni mwa mambo mengine, kwa vitendo vya ushoga.
Waziri wa mambo ya nje wa Uganda Okello Oryem ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba kuna njama ya mapinduzi inayofanywa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani, ambayo anasema inaongozwa na watu wanaohimiza ajenda ya jamii ya LGBT Afrika.
Oryem anahoji, “kwanini wasipitishe vikwazo kama hivyo katika nchi za Mashariki ya Kati ambazo zina sheria sawa au hata kali dhidi ya LGBT? “Ikiwa wanakata kuwapiatia visa wabunge wetu, basi watakwenda Shangai, Guangzhou, na kuna maeneo mengine mengi mazuri kutembelea”
Marekani iliweka duru ya kwanza ya marufuku kwa maafisa wa Uganda kujibu sheria mwezi June na Benki Kuu ya Dunia ilisitisha mikopo kwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki mwezi Ogusti.