Mkuu wa mkoa Morogoro amewatembelea wahanga wa mafuriko kata za Rudewa na Mvumi Wilayani Kilosa baada ya usiku wa kuamkia Disemba. 5 mwaka huu kutokea mafuriko katika maeneo hayo na kusababisha Kaya zaidi ya 300 kukosa makazi na vifo vya watu wawili
Rc Malima amefika na kukagua eneo la kingo za mto Wami ambazo baada ya kukatika maji yakaingia katika makazi ya watu kata ya Mvumi ambapo amewataka wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita sitini kwenye mito
Anasema baada ya kufanya ukaguzi amegundua shughuli za kibinadamu nazo zimechangia kingo za mto kukatika hivyo wananchi wanatakiwa kuheshimu sheria za utunzaji mazingira kwani athari zake ni kubwa sanaa ikiwemo kutokea mafuriko.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amesema baada ya kutokea mafuriko wametenga Sehemu maalum kwa ajili ya wahanga hao kujihifadhi wakati taratibu zingine zikiendelea.
“mhe. Mkuu wa Mkoa kila kata tumetenga Sehemu za kuwahifadhi wahanga wa mafuriko ili wawese kulala kwani wengine nyumba zao zimebomoka kabisa”
Usiku wa kuamkia Disemba 5 mwaka huu Wilaya Kilosa ilikumbwa na mafuriko kwenye kata za Mkwatani,Mvumi na Rudewa baada ya kubwa kinyesha katika mikoa ya Manyara na Dodoma na kusababisha vifo vya watu wawili na kaya zaidi ya mia tatu kukosa makazi.