Mashambulizi ya Israel yameongezeka katika eneo lote la Ukanda wa Gaza, hasa katika maeneo ya karibu na hospitali na sehemu ya kusini ya eneo hilo lililozingirwa, ambapo operesheni za ardhini zinaongezeka, iliripoti Al Jazeera.
Kwa mujibu wa takwimu za hivi punde zaidi za majeruhi zilizotolewa na Wizara ya Afya ya Palestina, hadi tarehe 6 Disemba, 6:00am kwa saa za ndani (04:00 GMT), Wapalestina 16,510 wameuawa shahidi huko Gaza na Ukingo wa Magharibi, wakiwemo angalau watoto 7,112.
Zaidi ya hayo, angalau Wapalestina 46,981 wamejeruhiwa, Al Jazeera iliripoti.
Wakati huo huo, watu 1,147 wameuawa nchini Israel tangu Oktoba 7 huku 8,730 wakijeruhiwa, kwa mujibu wa Al Jazeera ikilinukuu jeshi la Israel.
Viongozi mnamo Novemba 10 walirekebisha idadi ya vifo kutoka 1,405 hadi “karibu 1,200”.