Mwimbaji maarufu wa Marekani, Sean Combs, almaarufu Diddy, amefunguliwa tena mashtaka ya unyanyasaji wa kijinsia na mwanamke mwingine, na hivyo kuwa wa nne katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja.
Mshtaki wa nne, Jane Doe, siku ya Jumatano, alidai kwamba “alisafirishwa kwa ngono” na “kubakwa na genge” mnamo 2003 na Diddy, Harve Pierre, rais wa zamani wa Bad Boy Records na mwanamume mwingine alipokuwa na umri wa miaka 17.
Akijibu hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diddy alisema, “Imetosha. Kwa wiki kadhaa zilizopita, nimekaa kimya na kutazama watu wakijaribu kuharibu sifa na urithi wangu.
“Madai ya kuudhi yametolewa dhidi yangu na watu binafsi wanaotafuta siku ya malipo ya haraka.
“Niseme wazi kabisa kwamba sikufanya kitu chochote kinachodaiwa. Na nitapigania jina langu, familia na ukweli.”