Mwimbaji wa Afrika Kusini Tyla Laura Seethal, anayejulikana kwa jina la Tyla, ameeleza kwa nini anampenda mwimbaji wa Nigeria Asake.
Akizungumzia msukumo wa wimbo wake maarufu wa ‘Water’ katika mahojiano ya hivi majuzi na RollingStone, Tyla alisema anapenda jinsi Asake anavyotumia “sauti zake za kwaya.”
Alisema wimbo wake ‘Water’ ulichochewa na Amapiano kutoka nchi yake ya asili, mvuto wake wa R&B wa utotoni na Afrobeats za Nigeria.
Alisema, “Muziki wa Amapiano ndio msingi wake [‘water’] kwa maoni yangu. Na ushawishi wote kutoka kukua kama Rihanna na wasichana wote wa R&B, wavulana wa R&B,na pop. Aina hiyo ya ushawishi ninaopenda kuleta katika muziki wangu.
“Kitu ninachopenda sana katika muziki wa Afrobeats ni wakati ninasikia sauti zilizopangwa zinazosikika kama kwaya, ukiskiza karibu.
Na ninapenda sana jinsi Asake anavyoitumia muundo wake wa muziki .
Mimi hupenda tu jinsi inavyosikika. kwa mfumo kama kwanya ndiomaana wimbo wangu ‘water,’ niliiingiza muundo huo.
Ni wazi, watu hawawezi kuacha kuimba, hawawezi kuiondoa akilini mwao, nyimbp ambayo ninaipenda.