Wabunge wa Urusi Alhamisi walipitisha azimio la kupanga uchaguzi ujao wa rais wa nchi hiyo Machi 17, 2024.
Maseneta wote 162 waliohudhuria katika Baraza la Shirikisho lenye wanachama 178, baraza la juu la bunge, walipigia kura azimio hilo katika jiji kuu la Moscow.
Vladimir Putin, kiongozi wa Urusi tangu 1999, kama rais au waziri mkuu, hajatangaza nia yake ya kugombea muhula mwingine, lakini anatarajiwa.
Chini ya mageuzi ya kikatiba yaliyopitishwa mwaka 2020, Putin, 71, anastahili kuhudumu mihula miwili zaidi ya miaka sita, ikimaanisha kuwa anaweza kusalia madarakani hadi 2036.
Licha ya vikwazo vya Magharibi kutokana na vita vya Ukraine, ambavyo sasa ni miezi 2 1/2 kabla ya kuadhimisha mwaka wake wa pili, ikiwa Putin atatafuta muhula mwingine kama rais, anapendelewa zaidi kushinda.
Mnamo Septemba, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema kwamba ikiwa Putin ataamua kutafuta muhula mpya, “hakuna mtu atakayeweza kushindana nao katika nchi yetu katika hatua ya sasa.