Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro ametoa maagizo kwa baraka la michezo Tanzania kushirikiana na mamlaka ya bima Tanzania (TIRA) na kampuni za bima kuwakatia bima wanamichezo kwani wapo kwenye hatari ya kuumia wawapo michezoni.
Dkt Ndumbaro ameyasema hayo akishiriki katika halfa ya uzinduzi wa tarifa ya utendaji ya soko la bima kwa mwaka 2022 iliyofanyika katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
Katika taarifa hiyo iliyosomwa na Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware ilibainisha mafanikio ya soko la bima ambayo ni pamoja na kuongezeka kwa Kampuni za Bima kutoka 33 mpaka kufika Kampuni 40 zikiwemo na Bima Mtawanyo kuongezeka kwa Mawakala wa Bima, kuongezeka kwa Washauri wa Bima pamoja na Watakwimu Bima
Aidha Dkt. Saqware ameweka wazi kuwa sekta Bima pia imechangia pato la Serikali kiasi cha aslilimia 1.68 kwa mwaka 2022
TAZAMA PIA :”IFIKAPO JANUARI KILA MCHEZAJI AWE NA BIMA” WAZIRI NDUMBARO AKIZINDUA TAARIFA YA SOKO LA BIMA KWA 2022