Ikidhihirisha dhamira yake ya maendeleo ya jamii, shirika la Vivo energy Tanzania, kampuni inayoongoza ya mauzo ya vilainisho vya Shell na Engen, wametoa mchango kwa shule ya Sekondari ya Jangwani, mchango unaoendana na misingi ya shirika hilo ya uwajibikaji kwa jamii katika Nyanja za elimu, afya na nishati endelevu.
Vivo energy Tanzania ilishirikiana na Shule ya Sekondari ya Jangwani kutatua changamoto wanazokumbana nazo wanafunzi wenye mahitaji maalum, ikiwa na lengo la kurahisisha mafunzo ya wanafunzi hao Pamoja na kujenga mazingira shirikishi shuleni.
Mchango huo, ikiwa ni magongo, pedi za kike, viungo bandia na nepi za watu wazima, ulitolewa katika maeneo ya Shule ya Sekondari ya Jangwani. Shughuli ilianza kwa mapokezi na utambulisho uliyotolewa na Makamu mwalimu mkuu wa shule, Paulina Aweda kwa niaba ya Mwalimu mkuu, Mama Bhoke, ambaye aliwashukuru kampuni ya Vivo Energy kwa kurudisha kwa jamii, Shule yetu ina wanafunzi wenye uhitaji maalumu 100, kati yao 82 ni wa Bweni na 18 wa Kutwa kuanzia kidato cha kwanza hadi sita, huwa wanakumbaa na changamoto ya vifaa kama vile Magongo, Mafuta maalum, Baskeli, Komputa kwa ajili ya kujifunzia, Magodoro, Miguu bandia n.k. Naomba nichukue fursa hii kuwakaribisha wadau wengine waje shuleni kwetu kutoa misaada.
Bw. Mohamed Bougriba, Mkurugenzi Mkuu wa Vivo energy, alitoa hutuba yenye ushawishi mkubwa akisistiza azma ya kampuni hiyo ya kuboresha Maisha ya wanafunzi, hususan wale wanao kumbana na changamoto. Juhudi hizi za ushirikiano zinaashiria mfano bora wa ujumuishaji wa uwajibikaji kwa jamii kwa mashirika binafsi na ushiriki wa jamii yenyewe, na kuonyesha uwezo mkubwa wa ushirikiano kuleta mabadiliko makubwa.
Shughuli ilifikia hitimisho wakati wanafunzi walipotoa shukurani zao, wakitambua nafasi muhimu ya shirika la Vivo Energy Tanzania katika kuwasaidia katika safari zao kielimu. Mradi huu unangazia umuhimu wa uwajibikaji kwa jamii kwa mashirika kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Vivo Energy Tanzania imedhamiria kuendelea kuwa na nafasi muhimu katika jamii. Mchango huu kwa Shule ya Sekondari ya jangwani ni mfano wa msimamo wa kampuni kujenga ushirkishwaji na elimu, kuchangia maendeleo ya jamii na kuhakikisha mafanikio kwa wanafunzi wote.