Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amevitaka vyama vya siasa nchini kushiriki kwa pamoja katika mijadala na kutoa maoni katika kuandaa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa maendeleo ya watanzania wote ili Taifa liwe na mwelekeo wa pamoja.
Profesa Mkumbo amesema hayo wakati akizungumza na waandisihi wa Habari kuelekea maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania bara unaoambatana na Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete na mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Tunaandika Dira ya Taifa sio Dira ya Serikali kwa hivyo Taifa hili nilakwetu wote tunataka tukubaliane tunakwenda wapi na kama safari yetu ni Mwanza basi taifa wote tukubaliane tunakwenda Mwanza halafu sisi vyama vya siasa tubishane namna ya kwenda Mwanza mwingine atasema mi nawapeleka kwa ndege,mwingine kwa treni na mwingine kwa mguu ili wananchi waweze kuchagua mikakati maana ya tunakwenda wapi ningetamani watanzania wote tuwe na mwelelkeo mmoja” Prof. Kitila Mkumbo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji