Zaidi ya wanajeshi 100 wa Israel wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya ardhini ya Israel mjini Gaza.
Watatu kati ya wanne waliotangazwa kufariki asubuhi ya leo waliuawa katika mapigano kusini mwa Gaza, huku wa nne akifariki katika ajali ya gari inayohusiana na kijeshi, Jeshi la Ulinzi la Israel linasema.
IDF imechapisha majina ya wanajeshi 430 waliouawa tangu mashambulizi ya Hamas tarehe 7 Oktoba.
Wanajeshi 101 wameuawa tangu IDF ilipoanza mashambulizi yake makubwa ya ardhini huko Gaza tarehe 27 Oktoba, ambayo yameendelea tangu – isipokuwa wakati wa usitishaji vita wa siku saba ambao ulimalizika tarehe 1 Desemba.