Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeeleza wasiwasi juu ya kuongezeka kwa vurugu katika sehemu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambazo zimesababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao kwenye eneo la Masisi, mkoa wa Kivu Kaskazini nchini humo.
OCHA imesema moja ya vijiji vilivyoathirika na vurugu hizo ni Bihambwe, ambacho maelfu ya wanaume, wanawake na watoto walitafuta hifadhi kutokana na vurugu za awali.
Ofisi hiyo imesema wafanyakazi wa mashirika ya kibinadamu wanakumbwa na vizuizi vikubwa katika kutoa misaada kwenye eneo hilo, na kwamba barabara inayounganisha Goma na katikati ya mji wa Masisi imefungwa.
“Familia hizo zimeleta mahitaji duni walipokuwa wakikimbia. Wanakosa kila kitu: huduma za afya, malazi, chakula, maji, vyoo,” anasema Dk Mashako.
Kulingana na mamlaka ya mkoa, kufikia tarehe 3 Novemba, angalau watu 74,000 wanahitaji msaada nje kidogo ya Goma kufuatia kuhama kwa watu wengi hivi karibuni. Inabakia kuwa ngumu sana kujua ni watu wangapi wamefika katika siku zilizopita, kwani waliofika wamekuwa wengi na ghafla.