Mwandishi wa vyombo vya habari na mtangazaji wa zamani wa kipindi cha mazungumzo\talk show Oprah Winfrey picha yake ilizinduliwa rasmi katika Matunzio ya Kitaifa ya Picha ya Smithsonian Jumatano, na kuongeza kufanana kwake na mkusanyo wa watu wa kihistoria wa Marekani.
Winfrey, mtangazaji wa kipindi cha muda mrefu cha ‘The Oprah Winfrey Show,’ pamoja na mfanyabiashara na mwanahisani, alisema hakuwahi kuwa na ndoto ya kuwa na picha yake kwenye jumba la makumbusho la Washington.
“Kati ya ndoto zote nilizokuwa nazo, sikujua hata kulikuwa na jumba la sanaa la kitaifa,” alisema kwenye hafla ya uzinduzi, akimaanisha utoto wake kukua katika umaskini, baada ya kuona picha hiyo kwa mara ya kwanza. “Ninaishi na kupumua ndoto ya Mungu kwangu leo.”
Picha hiyo, iliyochorwa na msanii wa Chicago, Shawn Michael Warren, inaonyesha Winfrey akiwa amevalia gauni la zambarau akiwa amesimama nje kando ya mti.
Picha yake inaungana na ile ya Wamarekani wengine mashuhuri, akiwemo Harriet Tubman, Rais Abraham Lincoln, Rais wa zamani Barack Obama na mke wa rais wa zamani Michelle Obama.