Sifa na umaarufu wa Diddy imeshuka sana katika wiki chache zilizopita baada ya kushutumiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia na pande nne tofauti, moja baada ya nyingine – na kwamba, biashara zake pia zimepata pigo.
Siku ya Jumatano (Desemba 13), Variety iliripoti kwamba Hulu sasa amekatiza uhusiano na mogul huyo wa Bay Boy Records baada ya hapo awali kufanya naye kazi kwenye kipindi chake cha televisheni \reality show inayokwenda kwa jina la Diddy+7, ambayo ilikuwa bado katika hatua zake za awali, ili kuelezea maisha ya familia yake
Baada ya kupata mkataba wa uzalishaji na kampuni ya James Corden, Fulwell 73, project hiyo sasa umefutiliwa mbali kabisa.
Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 54 ameripotiwa kupoteza ushirikiano mwingi wa aina hiyo tangu madai hayo yaanze kuongezeka.
Kwa jumla, kampuni 18 zimeachana na tovuti yake ya e-commerce, Empower Global.
Kulingana na ripoti ya Rolling Stone, washirika wengi wametaja shida za kisheria za Diddy kama sababu ya kujiondoa kwenye mradi huo.
“Uamuzi huu ulifanywa siku ambayo Casandra Ventura aliwasilisha kesi yake,” alisema. “Tunachukulia madai dhidi ya Bw. Combs kwa uzito mkubwa na tunaona tabia kama hiyo kuwa ya kuchukiza na isiyovumilika tunaamini katika haki za wahasiriwa, na tunaunga mkono waathiriwa katika kusema ukweli wao, hata dhidi ya watu wenye nguvu zaidi.
Lenard Grier wa kampuni ya No One Clothiers, aliongeza: “Ingawa uamuzi huu ulikuwa mgumu kwa sababu [ya] staha tuliyokuwa nayo wakati mmoja kwa Bw. Combs kama kiongozi katika biashara na burudani, kwa wazi lilikuwa chaguo sahihi.”