Kampuni ya uzalishaji wa vifaa vya ujenzi ya Knauf Gypsum Tanzania imeungana na Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kutoa msaada wa vifaavya ujenzi kwa wakazi wa Hanang walioathiriwa namafuriko na maporomoko ya mlima yaliyosababishavifo vya watu 89.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na gypsum boards,skimming plasters ambavyo vitatumika kusaidiaujenzi wa majengo yaliyoharibika.
Akiongea wakati wa kukabidhiwa msaada huo jijiniDar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Gilead Teri alisema hatua ya kuwasaidia wakazi wa Hanangwalioathiriwa na maafa iliyochukuliwa na Knauf Gypsum Tanzania ni ya kupongezwa na kuwatakawawekezaji wengine kuiga mfano.
“Kampuni ya Knauf imekuwa ndiyo ya kwanza kutufikia na kutueleza nia yao ya kutaka kuwasaidiawakazi wa Hanang. Baada ya kutufikia na sisituliwasiliana na ofisi ya Waziri inayohusika namazingira ili kuweza kufikisha msaada kwawaathirika wa mafuriko na maporomoko,” alisema
Aliongeza “Huu ni mfano mzuri na bora kabisa kwamakampuni mengine kuiga kwa kuwa unaonyeshanamna wanavyojali na kushirikiana na jamii hatawakati wa majanga na shida. Hii inakwendasambamba na ule msemo wa Rafiki anayekujaliwakati wa shinda ndiyo Rafiki wa kweli. Leo Knauf imetuonyesha kuwa ni Rafiki wa kweli,”
Kwa upande wake mkurugenzi wa Knauf Gypsum Tanzania Ilse Boshoff alielezea kampuni hiyokuguswa na tukio la Hanang na kuona umuhimu wakutoa msaada kwa jamii na wakazi wa eneo hilo nakuongeza kuwa kampuni hiyo ipo tayari kushirikianana Watanzania katika hali zote.
“Tunajisikia furaha kufanya kazi na Serikali yaTanzania kwa ajili ya kusaidia maendeleo yaWatanzania. Kwa namna ya pekee, leo tunayo furahakutoa msaada huu kwa wakazi wa Hanangutakaosaidia ujenzi wa majengo yaliyoharibiwa,” alisema