Kuelekea Hafla ya Utiaji Saini Mikataba ya Usanifu wa Miradi ya Uboreshaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) Kwa Miji 15 ya Kundi la Pili (Tier 2) itakayofanyika Mjini Bukoba Mkoani Kagera kesho Tarehe 15,Disemba 2023.
Kikundi-kazi cha Utekelezaji wa Miradi inayotekelezwa kwa Ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais @ortamisemitz na Benki ya Dunia kupitia @TaruraTz kimetembelea maeneo ya miradi itakayotekelezwa Mjini Bukoba.
Miradi itakayotekelezwa Bukoba ni Ujenzi wa Stendi Mpya ya Kisasa Kyakailabwa, Barabara za Lami Kilomita (7),ufungaji wa taa za umeme wa jua, Ujenzi wa Soko kubwa la kisasa na Ujenzi wa Mto Kanoni wenye urefu wa KM 7.3.