Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa Pikipiki aina ya Bajaji kwa Bw. Leonard Msirikale mwenye ulemavu wa uti wa mgongo ikiwa ni agizo lake alilolitoa siku ya wafanyakazi Dunia (Mei mosi) 2022 mkoani Morogoro la kumpa msaada wa kujikwamua kiuchumi.
Msaidizi wa Rais maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Rais Ikulu, Felister P. Mdemu ameikabidhi pikipiki hiyo mkoani Morogoro kwa niaba ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.