Kikosi cha Liverpool kilikamilisha kampeni yake ya hatua ya makundi ya Ligi ya Europa kwa kufungwa 2-1 na Union St.-Gilloise nchini Ubelgiji siku ya Alhamisi.
Wakiwa na pointi 12, Liverpool tayari walikuwa wamejihakikishia nafasi ya kwanza katika Kundi E na kutinga katika hatua ya 16 bora katika michuano ya sekondari ya Ulaya.
Licha ya ushindi huo, Union ilishindwa kupata nafasi ya pili na kufuzu kwa hatua ya mtoano huku Toulouse ikiifunga LASK Linz katika mchezo mwingine wa mwisho wa kundi hilo badala yake Union italazimika kushika nafasi ya tatu kwenye kundi na kuangukia katika mchujo wa mtoano wa Ligi ya Europa Conference.
Mohamed Amoura aliifungia Union bao la kuongoza kwa shuti kali dakika ya 32 baada ya kumpata kipa wa Liverpool Caoimhin Kelleher.
Liverpool, hata hivyo, ilichukua dakika saba pekee kupata bao kupitia kwa Jarell Quansah ,beki huyo mwenye umri wa miaka 20 alikusanya kona kutoka kwa Curtis Jones ndani tu ya eneo la hatari na kuachia shuti kali hadi wavuni kwa bao lake la kwanza la Liverpool.