Kufuatia mafanikio mengi na kukubalika kwa project yake ya mwisho la ‘Holy Ghost’ na mashabiki katika sehemu mbalimbali za dunia,wa mwimbaji aliyeshinda tuzo nyingi Omah Lay anatazamiwa kuachia wimbo mpya kabla ya mwaka wa 2023 kukamilika.
Mwimbaji huyo ametoa tangazo hili na uthibitisho katika chapisho aliloliandika kwenye mtandao wake wa kijamii siku ya Alhamisi, Desemba 14, 2023, kwamba atatoa wimbo mpya kabla ya mwaka kuisha, hii itakuwa ni yake ya pili kuiachia baada ya toleo lake la deluxe la albamu yake ya kwanza, Boy Alone.
Omah Lay alitangaza kuwa atatoa wimbo mpya ili mashabiki waufurahie siku ya Ijumaa, Desemba 15, 2023. Tangazo hilo liliwashangaza wengi huku wengine wakikisia kwamba huenda mwimbaji huyo yuko njiani kuachia albamu mpya kwa EP katika robo ya kwanza ya 2024.