Vita huko Gaza vitapita kwenye awamu mpya inayolenga shabaha sahihi ya uongozi wa Hamas na operesheni zinazoendeshwa kijasusi, Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan alisema Ijumaa huko Israel.
Sullivan hakutoa maelezo juu ya muda wa mabadiliko katika nguvu ya vita.
“Mazingira na muda wa jambo hilo kwa hakika lilikuwa suala la mazungumzo niliyokuwa nayo na Waziri Mkuu Netanyahu,” baraza la mawaziri la vita, viongozi wa kijeshi wa Israel na waziri wa ulinzi, Sullivan alisema katika mkutano na waandishi wa habari.
Sullivan aliongeza kuwa Marekani iko kinyume na mpango wowote ambao ungeiona Israel ikiikalia Gaza kwa muda mrefu, huku uvumi ukiongezeka juu ya mustakabali wa baada ya vita wa eneo hilo.
“Hatuamini kwamba ina maana kwa Israel, au ni sawa kwa Israel, kuikalia Gaza, kuikalia tena Gaza kwa muda mrefu,” Sullivan aliwaambia waandishi wa habari huko Tel Aviv.