Katika kuunga mkono juhudi za Serikali, kusaidia waathiirika wa mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya tope,mawe na maji katika mji wa katesh wilayani Hanang mkoani Manyara,Shirika lisilo la kiserikali la AMO FOUNDATION limefika wilayani humo.
Shirika Hilo la AMO FOUNDATION limefika na kutoa misaada Kwa waathiirika wa Mafuriko, ambopo Afisa mahusiano wa shirika hilo Ramadhan Rajabu amesema wamekuja kumuwakilisha mkurugenzi wao Amina Said ambaye Kwasasa Yuko nje ya nchi na Shirika hilo limetoa unga wa sembe Tani tatu (3) Maharage tani Moja (1) pamoja na mafuta ya kupikia.
Nae Naibu Waziri wa Ujenzi Geofrey Kasekenya amewaomba wadau wenye nia ya kuendelea kutoa misaada ya hali na mali wilayani Hanang kwaajili ya waathirika wa tope kuweka kipaombele vifaa vya ujenzi ili kusaidia kutimiza lengo na takwa la Rais Samia Suluhu Hassan la kuwajengea makazi waathirika.
Huku Afisa Mahusiano wa taasisi hiyo Ramadhan Rajabu akisema taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali kwa nyakati zote kuhakikisha wanarejesha tabasamu kwa wananchi wa Hanang