Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) limewataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan kutembele Hifadhi za Taifa mbalimbali zilizopo karibu ili kuongeza Pato la Taifa kupitia sekta ya utalii Kwa kuanzisha Kampeni ya “TWENZETU MBUGANI”
Akizungumza na waandishi wa Habari kaimu Kamishna wa Uhifadhi (TANAPA) Juma Kuji amesema kipindi hiki Cha sikukuu Watanzania wanatakiwa kutumia muda huu wa mapumziko kutembele Hifadhi na kuhamasisha Jamii kujifunza mambo mbalimbali kwenye sekta hiyo
Kuji amesema ni muda muafaka Kwa kuendelea kumuunga Mkoa Rais Samia kupitia filamu ya The Royal Tour kuhamasisha utalii wa ndani badala ya kutegema Watalii kutoa nje ya nchi ambapo amebainisha Kuna Hifadhi 21 nchini zenye vivutio vya kipekee
Amesema sekta ya utalii inachangia kiasi kikubwa cha fedha kwenye Pato la Taifa hivyo serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya hifadhi .
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wakizungunza na Ayo na Millard Ayo .com Kwa nyakati tofauti wamesema watu wengi hawana Muamko wa kutembele Hifadhi kutalii wengi wakiona ni jambo la Watalii kutoka nje ya nchi.
Wanasema kupitia elimu inayotolewa na TANAPA Kwa sasa muamko unaongezeka wa Watanzania Kupenda kutalii kwenye hifadhi za Taifa tofauti na kipindi Cha nyuma.